Kwa Nini Kuweka Alama Ya Utambulisho Isiyofutika Kwenye Vipuri Vya Gari Yako (Direct Part Marking) Ni Muhimu Kwa Tanzania Na Barani Afrika.
Fikiria umeegesha gari lako nje ya mgahawa wenye shughuli nyingi jijini Dar es Salaam au unahudhuria ibada ya Jumapili jijini Arusha au umeegesha gari unawashusha watoto wako shuleni jijini Mwanza, au umeegesha gari la kazi la kampuni usiku kucha kwenye eneo unahisi kuna usalama jijini Dodoma. Unaporudi, kila kitu kinaonekana salama. Milango imefungwa, vioo vimepandishwa,…
